
Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye
Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 22, 2022, mkoani Manyara, ambapo Rais Samia yuko mkoani humo kwa ajili ya ziara ya siku mbili.
"Mimi kama mzee wa mkoa huu, ambacho nimemuambia Mwenyekiti mpya, kazi kubwa ya chama ni kuhakikisha CCM inaendelea kuongoza dola katika nchi yetu ya Tanzania, Mhe. Rais nakuhakikishia sio kuongoza dola tu na hiyo bendera tutaendelea kukukabidhi wewe uongoze nchi yetu mpaka 2030," amesema Waziri Mstaafu Sumaye
Aidha Sumaye ameongeza kuwa "Wale wenye upeo wa kuangalia mbali kidogo kwa nchi yetu, Mama Samia anafanya mambo makubwa kwa Taifa hili na faida yake tutaiona hivi karibuni mbele tunakokwenda,Mh. Rais tutakusimamia na si kwa sababu yoyote ila kwa sababu unapiga kazi kwa ajili ya Watanzania wa ngazi zote,".