Jumapili , 19th Jul , 2020

Rais John Magufuli amefanya mabadiliko ya uteuzi Mkoa wa Njombe kwa kumteua Mhandisi Marwa Mwita Rubirya kuwa Mkuu wa mkoa wa Njombe.

Rais Magufuli

Rubirya ameteuliwa badala ya Bw. Jumanne Fhika ambaye aliteuliwa Julai 17, 2020 lakini sasa atabaki Ofisi ya Rais kuendelea na majukumu yake. 

Kabla ya uteuzi Rubirya alikuwa Meneja wa TANROADS mkoa wa Mwanza.