Rais Magufuli amfanyia dua Rais Mwinyi

Jumatano , 5th Dec , 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Desemba 5, 2018, amemtembelea na kumjulia hali Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli akiwa kwenye dua na familia ya Rais mstaafu Mwinyi.

Pamoja na Kumjulia hali, Rais Dkt. John Magufuli ameshiriki dua ya kumuombea Afya Njema iliyoongozwa na familia ya Rais huyo mstaafu.

Walioshiriki wa Dua hiyo Maalumu ni Rais Magufuli mwenyewe, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Bi. Sitti Mwinyi (Mke wa Mzee Mwinyi) pamoja na Abdallah Mwinyi (Mtoto wa Mzee Mwinyi).

Rais Magufuli ameiaga familia hiyo kwa kuwapa moyo kuwa mzee Mwinyi atarejea kwenye hali yake ya kawaida na kikubwa waendelee kumuombea tu.

Taarifa zaidi bado hazijaelezwa kuwa ni ugonjwa gani unamsumbua Rais Mwinyi.