
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa.
Rais Magufuli ametoa pongezi hizo katika misa takatifu ya shukrani ya uhai kwa Rais Mstaafu Mkapa ametimiza miaka 80 tangu kuzaliwa iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Upanga Jijini Dar es Salaam.
"Mhe. Rais Mstaafu Mkapa wakati wa uongozi wako ulifanya kazi kubwa, na kwa miaka 20 ambayo nilifanya kazi na wewe baada ya kuniteua kuwa Naibu Waziri na baadaye Waziri nilijifunza kuwa wewe ni mcha Mungu, muadilifu, mnyenyekevu kwa Mungu na mchapakazi."
"Leo unapotimiza miaka 80 nakushukuru na kukupongeza sana, nakuombea Mwenyezi Mungu aendelee kukupa afya njema wewe na familia yako, na sisi viongozi tuliopo sasa tutaendelea kuyaenzi mazuri yote uliyoyafanya" amesema Mhe. Rais Magufuli.
Rais Mstaafu Mkapa amebainisha kuwa anampongeza Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi wake kwa kuwa Tanzania imeendelea kuwa na sifa nzuri ya amani na umoja na kwamba hata akiwa nje ya nchi anapoulizwa siri ya Tanzania kuwa na amani.