Rais Magufuli ampa shavu Mkapa

Jumanne , 14th Mei , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, amemteua Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM).

Uamuzi huo wa Rais Magufuli ameutangaza leo kupitia taarifa yake iliyotumwa kwa vyombo vya habari ambapo anashika nafasi hiyo kwa awamu ya pili mfululizo.

Aidha kwenye uteuzi huo Rais Magufuli amemteua Profesa Ignas Rubaratuka kwenye Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

April 4, 2019 akiwa ziarani mkoani Mtwara Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amesema hatajali maneno ya watu ambao watasema kuwa yeye anajenga miundombinu kwenye Mkoa anaotoka Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa, kwa kuwa anajua alipotoka naye.