Alhamisi , 8th Nov , 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amelitaka jopo la madaktari na wataalamu wa masuala ya moyo kutoka Israel kutenga muda maalum kwa ajili ya kutembelea baadhi ya vivutio vya utalii hapa nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Akizungumza na jopo hilo la madaktari Ikulu Jijini Dar es salaam Rais Magufuli ametangaza kuwapa siku 3 wataalamu hao kwa ajili ya kwenda kufurahia kwenye mbuga ya Serengeti na Ngorongoro.

Niwaombe mtenge siku 2 au siku 3 tuwapeleke kwenye mbuga zetu hamtalipa chochote, ofa ni kutoka kwetu na kama mtakubali mi nawapa ofa, kwa ajili ya kuwapa muda kupumzika kwa sababu mtakuwa mmefanya kazi kubwa ya kushughulika na masuala ya moyo.”

Wataalamu hao wamekuja nchini kwa ajili ya kutoa huduma za bure za moyo, pamoja na kutoa mafunzo kwa madaktari nchini ambapo Rais Magufuli aliishukuru Israel kwa mafunzo hayo na kuongeza serikali inafanya juhudi mbalimbali za kuhakikisha inaboresha huduma za afya nchini.

Tanzania itaendelea kushirikiana na Israel, itashirikiana na Marekani na ndiyo maana katika awamu hii niliamua kufungua Ubalozi kwa makusudi wa Israel, urafiki kati ya Tanzania na Israel utaendelea kudumu