Ijumaa , 7th Jun , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 30, kwa baadhi ya makampuni ambayo yamekuwa yakijihusisha na ukwepaji kodi, kwa kuanzisha Makampuni hewa ya nje na baadaye kuomba punguzo la bei ya thamani kwa bidhaa wanazoziuza nje ya nchi.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo katika mkutano wake na wafanyabiashara kutoka Wilaya 139 nchi nzima, ambao amewaita jijini Dar es salaam kwa ajili ya kujadili changamoto za biashara nchini.

Rais Magufuli amesema kuwa "nimefuatilia baadhi ya wafanyabiashara wanatumia mbinu mbalimbali kukwepa kodi, kwa kudai marejesho ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT), wakati mauzo yaliyofanyika ni mauzo hewa kutoka kwa Makampuni ya nje, nina orodha ya Makampuni 17,446, ambayo yamehusika na tuhuma hizi''.

"Sijui nani kiongozi wenu ila tukimaliza nitawapa orodha ili Makampuni hayo mkafanyae uchambuzi wenu ili na yale makampuni yatakayobainika yakajipange kulipa ndani ya siku 30." - amesema Rais Magufuli.

Leo Rais Magufuli amekutana na wafanya biashara watano kutoka kila wilaya nchini ambao wamewawakilisha wenzao, lengo ikiwa ni kufahamu matatizo yanayowapata.