
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bw. Gerson Msigwa, na kuichapisha kwenye ukurasa wake wa twitter.
Magufuli ateua Kamishna TRA
Pia Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Kamishna Mkuu wa TRA nchini ambapo nafasi hiyo ilikuwa ikisimamiwa na Bw. Charles Edward Kichere, na kumteua Bw. Edwin Mhede kushika nafasi hiyo.
Kabla ya uteuzi huo Mh. Inocent Lugha Bashungwa alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo, na Bw. Mhede alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara.
Kamishna MKuu mpya wa TRA Bw. Edwin Mhede (Kushoto) Mh. Innocent Lugha Bashungwa (kulia)
Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara utafanyika baadaye.
Isome zaidi hapa
