Jumapili , 8th Dec , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, ametuma salamu za pole kwa familia ya Ali Mufuruki, aliyeaga Dunia nchini Afrika Kusini, wakati akifanyiwa matibabu katika Hospitali ya Morningside, Jijini Johannesburg.

Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, kulia ni Marehemu Ali Mufuruki.

Rais Magufuli ametuma salamu zake za pole leo Decemba 8, 2019, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.

"Nimehuzunishwa na taarifa za kifo cha rafiki yangu Ali Mufuruki (Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Jukwaa la Wakurugenzi Watendaji wa Kampuni - CEOrt), Nitamkumbuka kwa uzalendo na mchango wake katika kukuza sekta ya biashara na ushauri kwa Serikali.Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un" ameandika Rais Magufuli.

Ali Mufuruki amefariki usiku wa kuamkia leo Desemba 8, 2019.