Jumanne , 6th Aug , 2019

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amekemea baadhi ya kauli zinazotolewa na viongozi waliopo madarakani hivi sasa nchini humo, na kudai kuwa wanatoa kauli ambazo zinaashiria ubaguzi miongoni mwa Wamarekani.

Barack Obama ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye mahojiano na kituo cha habari cha Uingereza BBC, ambapo ameitaka Serikali ya Marekani kudhibiti suala la umiliki wa silaha kiholela miongoni mwa Wamarekani, ili kuepusha mauaji ya mara kwa mara.

"Inabidi kwa pamoja tukatae lugha na maneno yanayotolewa na baadhi ya viongozi wetu, ambayo yanasababisha mazingira ya uoga na chuki miongoni mwa Wamarekani, tuwakemee viongozi wanaotuaminisha kuwa wahamiaji wanaokuja Marekani, wanahatarisha maisha yetu." amesema Obama

Tangu atoke madarakani Barack Obama amekuwa sio mtu wa kuzungumza mara kwa mara, lakini huenda kauli yake hiyo imekuja kufuatia kutokea kwa mauaji ya kutumia silaha yalisababisha vifo vya watu 26, nchini humo, mnamo Agosti 4.