Jumanne , 3rd Mei , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amemtaka Waziri wa Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye, kuchuja katuni zinazopatikana mitandaoni kwani baadhi ya zilizopo zinakiuka mila na desturi za Mtanzania.

Kushoto ni Waziri wa Habari Nape Nnauye, na kulia ni Rais Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 3, 2022, mkoani Arusha wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari.

"Kuna katuni na watoto wanavyopenda, katuni zilizopo mitandaoni mwanaume kwa mwanaume wanabusiana, mwanamke kwa mwanamke wanashikana ni katuni ambazo hatuzi-control, Mhe. Waziri na Wizara yako hatuchuji hatuna chochote, hivi mila zinaruhusu watoto wetu waone hayo hatufikiri mpaka Rais aseme, kafanyeni kazi yenu," amesema Rais Samia