Jumatatu , 21st Jun , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo Juni 21, 2021, leo amezungumza kwa njia ya simu na Rais wa China Xi Jinping, ofisini kwake Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, ambapo China imeahidi kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Katika mazungumzo hayo Tanzania na China zimekubaliana kukuza ushirikiano katika nyanja za kiuchumi, utamaduni na ushirikiano wa Kimataifa, ambapo China pia imeahidi kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mbali na hayo pia Rais Xi Jinping, ametumia nafasi hiyo kumpa pole Rais Samia kwa kuondokewa na mtangulizi wake Hayati Dkt. John Magufuli, aliyefariki dunia Machi 17, 2021, kutokana na maradhi ya moyo yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.