Jumatano , 8th Sep , 2021

Rais Samia Suluhu Hassan leo Septemba 8, 2021, akiwa mkoani Mwanza amesimikwa kuwa Chifu wa machifu wote wa Tanzania na kupewa jina la Hangaya lenye maana ya kwamba ni Nyota Inayong'aa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Hayo yamejiri wakati alipohudhuria Tamasha la Utamaduni mkoani Mwanza lililoandaliwa na Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) na Kituo cha Makumbusho cha Bujora Mwanza, ambapo mara baada ya kusimikwa alisema,

"Nashukuru sana umoja wa Machifu na Watemi kwa kunipa jina hili zuri sana, na ninamuomba Mwenyezi Mungu anijaalie niendane na jina hili, niwe kweli Nyota Inayong'ara na kung'ara huku sio kuning'arisha mimi tu kunisaidie pia ning'arishe nchi yangu," amesema Rais Samia