Rais Samia Suluhu atengua uteuzi Mkurungezi TPDC

Jumatatu , 5th Apr , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. Thobias Mwesigwa Richard na kumrejesha Dk. James Mataragio.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Utenguzi wa Bw. Thobias umekuja muda mchache baada ya kuteuliwa Aprili 4, 2021.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa imeeleza kuwa Rais Mhe. Samia Suluhu amemrejesha Dk. James Mataragio kuendelea na majukumu.