Jumanne , 31st Jan , 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa licha ya wananchi wengine kupaogopa polisi lakini hata yeye pia kuingia mahakamani hata polisi anapaogopa kama sio sehemu ya kazi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 31, 2023, Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma, wakati akizindua Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai nchini.

"Mimi mwenyewe ukiniambia kuingia mahakamani kama si kwa kazi naogopa, naogopa tu, lile jengo la mahakama naliogopa, au polisi naiogopa, kwa sababu nikiingia polisi hata kama nina jambo kwenda kulishtaki mimi nilikuwa naogopa huko nyuma, niende polisi nikashtaki kwamba nimefikwa na hili mhh!! watanigeuzia siendi, au niambiwe sijui fulani ana kesi niende mahakamani siendi, hata kama kesi sio yangu," amesema Rais Samia

Aidha Rais Samia akasisitiza "Kwahiyo ni wangapi wanaogopa hayo majengo badala ya kuona kwamba ni maeneo ya kusaidiwa kupata haki zao watu tunaogopa kwenda hayo maeneo, kwahiyo tukayatizameni,"