
Waziri wa Mazingira na Nishati wa Ecuador Inés Manzano amewaambia waandishi wa habari kuwa Huko Cañar, kusini mwa Ecuador, "watu 500 walitokea na kuanza kurusha mawe kwenye msafara wa rais, na ni wazi, pia kuna matundu ya risasi kwenye gari la rais, huku akiweka wazi kuwa rais hakujeruhiwa.
Kwenye mtandao wa kijamii wa X, ofisi ya rais imeeleza kuwa ni "shambulio" na ikatoa video zinazoonyesha tukio hilo kutoka ndani ya gari moja kwenye msafara wa rais, huku mabomu kadhaa yaliyotengenezwa kienyeji yakigonga madirisha na mtu aliyekuwa ndani akipiga kelele
Picha nyingine zilizochukuliwa nje zilionyesha kundi la waandamanaji, wengine wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni, wakirusha mawe na fimbo kwenye msafara huo.
Mamlaka inachunguza iwapo athari zinazoonekana kwenye gari aina ya SUV lisiloingiza risasi lililokuwa limembeba kiongozi huyo zilisababishwa na urushaji risasi.
Msafara wa magari ulilengwa ulipokuwa ukielekea katika mji wa Andean wa Cañar (kusini mwa Ecuador).
Inés Manzano ameripoti kwamba serikali iliwasilisha malalamiko kwa "jaribio la mauaji" na kwamba watu watano wamekamatwa. Watachunguzwa kwa kosa la ugaidi, adhabu yake ni kifungo cha hadi miaka 30 jela.