Alhamisi , 7th Jul , 2022

Rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba amemuomba Vladimir Putin wa Urusi kulisaidia taifa lake lenye uhaba wa mafuta, kwa kuwa linakabiliwa na mgogoro mbaya zaidi wa kiuchumi tangu Sri Lanka ilipopata uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1948.

Rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa

Hatua hiyo inakuja baada ya waziri wa Nishati wa Sri Lanka kuonya mwishoni mwa wiki kwamba nchi hiyo huenda ikaishiwa na mafuta ya petroli. 

Siku ya Jumatano, mamia ya watu waliingia katika mitaa ya mji mkuu Colombo kuandamana dhidi ya serikali.
Bwana Rajapaksa pia amesema kuwa "ametoa ombi kwa unyenyekevu" kwa safari za ndege kati ya Moscow na Colombo kuanza tena, baada ya shirika la ndege la Urusi Aeroflot kusitisha huduma mwezi uliopita.