Jumatano , 28th Nov , 2018

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema kuwa wanaendelea kufanya mawasiliano na wataalamu wa jiolojia ili kuweza kubaini ni kitu gani kilichotokea usiku wa kuamkia leo mji ambacho kilisababisha kishindo kikubwa na muungurumo uliotanguliwa na mwanga mkali.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti

Tukio hilo ambalo wengi kupitia mitandao ya kijamii wamedai kuwa ni kimondo na kupelekea maelfu ya wakazi wa Kagera kutoka nje ya nyumba zao kwa kile walichokidhani kuwa ni tetemeko la ardhi kufuatia maafa waliyoyapata septemba 2016.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo, Brigedia Jenerali Gaguti amesema kuwa ameagiza serikali kuwasiliana na baadhi ya wataalamu kwenye mkoa huo ambapo hivi karibuni wanatarajia kutoa tamko kwa umma.

Wakati huohuo mgomo wa madereva wa magari ya abiria uliodumu kwa masaa kadhaa umepatiwa ufumbuzi, baada ya pande mbili zenye mgogoro ikiwemo manispaa  pamoja na madereva kukaa meza ya mazungumzo.

Kupitia Katibu tawala wilaya ya Bukoba Kadole Kilugala amesema kuwa katika kikao walichokaa na viongozi wa madereva na wadau wengine wa usafiri, walikubaliana masuala kadhaa ambayo madereva hao wanahitaji yafanyiwe kazi ikiwamo kituo hicho kuwekewa lami