
Aidha, Dk. Nawanda amemuagiza Mkuu wa Polisi pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo, Aswege Kaminyoge, kuwakamata watu wanaovamia na kulima maeneo ya shule wilayani humo
RC Nawanda ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Maswaqq, inayolenga kuzifikia wilaya zote za mkoani hapa
Akiwa katika Shule ya Sekondari Nyalikungu, Kinamwigulu, Buchambi na Zanzui, RC Nawanda ameonya kamwe hatapokea miradi yenye changamoto