Jumatano , 1st Mar , 2023

Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya, linamshikilia Regina Issack (40), anayedaiwa kuwa na matatizo ya akili, mkazi wa Ilindi, Kata ya Ilemi jijini Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake, Sisela Ngailo (09).

Polisi

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP,  Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limetokea Februari 23, 2023 majira ya saa 7:00 mchana ambapo Regina alimnyonga  shingo mwanae akiwa amelala.

"Chanzo cha tukio hili inasadikika mtuhumiwa kuwa na tatizo la afya ya akili ambapo alikuwa akihudhuria  matibabu ya afya katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH) tayari uchunguzi wa tukio hili unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika," amesema Kamanda Kuzaga.