Ijumaa , 13th Mei , 2022

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Kuitangaza Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi amesema filamu ya Royal Tour ni lango linalokwenda kufungua maendeleo kwenye kila sekta hapa nchini.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Kuitangaza Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi

Akizungumza leo Mei 13, 2022 kwenye Kikao cha 17 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali jijini Tanga. Dkt, Abbasi ametoa wito kwa Maafisa Habari kuitangaza  na amemkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali nakala ya filamu hiyo ili isambazwe nchini kupitia kwa maafisa hao.

Dkt.Abbasi amebainisha kuwa filamu hiyo inatarajiwa kutazamwa na zaidi ya watu bilioni moja katika kipindi kifupi huku akifafanua kuwa uzinduzi uliofanywa nchini Marekani ambako ni soko kuu la utalii wa Tanzania Rais Samia ameweza kukutana na viongozi matajiri katika sekta mbalimbali ambao wameonyesha nia ya kuwekeza hapa nchini.

Kauli mbiu ya kikao hicho ni " Mawasiliano ya Kimkakati nyenzo muhimu kufanikisha  sensa ya Watu na Makazi 2022"

Kikao kazi hicho kimefungwa rasmi na Waziri wa TAMISEMI Innocent Lugha Bashungwa ambaye amesisitiza Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kusemea mafanikio ya Serikali.