Jumanne , 18th Sep , 2018

Zama zinabadilika na maisha yanabadilika pia, limekuwa ni suala la kawaida hivi sasa kusikia mtu amemuua rafiki yake, ndugu yake, mke au familia yake yote tena kikatili kabisa .

Kwa mujibu wa shirika la Afya duniani (WHO), utafiti unaonesha watu takribani 1000,000 hupoteza maisha kila mwaka kwa kujiua, ambao ni sawa na watu 3000 kwa kila mwezi na mtu mmoja kila baada ya dakika 40. Vijana wenye umri miaka 15-25 ndiyo wanaoongoza kwa matukio hayo.

Hali hiyo iko pia katika nchi ya Tanzania, ambapo katika kipindi cha Funguka kunachoruka kupitia EATV na ukurasa wa Facebook, wadau mbalimbali wametoa sababu mbalimbali zinazochangia kukithiri kwa matukio hayo katika maeneo yao  kwenye mada iliyouliza “NINI SABABU INAYOPELEKEA KUKITHIRI KWA MATUKIO YA WATU KUJIUA NA KUUA FAMILIA ZAO” na haya ndiyo maoni yao.

Robius wa Mjungu: Wa Kagera, Karagwe tz. Zipo sababu nying zifuatzo ni baadhi, 1 ni kuwa na msongo wa mawazo, 2 ni kuwa na ugumu wa maisha, 3 ni kutokua na moyo wa subira, mfano mwanamfunz akiwa amefeli.

Kelvin John Nyamuga: Wa Mwanza, mi nafikiri mpaka mtu kufikia hatua hiyo kuna mambo yanamchanganya na pa kuyaweka hakuna au hakuna wa kushirikiana nae kimawazo!.

Katoto Ever:  Wa Kurasini, Polisi ufundi...huwa ni matatizo ya kisaikolojia maana bora ukutane na mtu mwenye tatizo la akili ni raisi kumgundua kwani anaweza kuvaa viatu kichwani ila ambaye hana tatizo la kisaikolojia sio raisi kumtambua kwani huwa yuko smart na hawa ndio wakishafanya tukio Jamii mzima itabaki ikishangaa.

Zainabu Issa Kibirity: Wa Mi naona mtu anachukua maamuz hayo kwa msongo wa mawazo na akifikiria hana wa kumpa msaada wala nini, sasa unafikiri hapo utatamani kuishi.

Camila Mroso: Ugumu wa maisha unachangia kwa kiasi kikubwa.

Hammy de Love: Wa Morogoro, #funguka ni tamaa tu za kifedha na ugomvi wa kijinga ndicho kinachosababisha watu wengi kujiua ama kuuwa wenzao.

Juniour Silver: Mimi naona ni ugumu wa maisha kwa sasa na pia ni kutokana na kutokuwana maelewano ndani ya familia, ugomvi ndani ya nafsi ya mtu na ukosefu wa elimu katika jamii. Toka pande za moshi, mabogini juniour a.k.a yakuza juniour 11.