Ijumaa , 6th Mei , 2022

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, na wenzake wawili baada ya kubaini kulikuwa na mapungufu katika mwenendo mzima wa kesi. 

Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya

Sabaya na wenzake walikata rufaa kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 30 iliyotolewa na Mahakama hiyo Oktoba 2021.

Mbali na Sabaya wengine waliokuwa wamehukumiwa miaka hiyo 30 ni Sylivester Nyegu na Daniel Mbura.