Jumapili , 18th Oct , 2020

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu, ametaja sababu Rais Dkt.John Pombe Magufuli kutokuudhuria mkutano wa sekta binafsi uliobeba lengo la kumpongeza kwa mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka mitano.

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu

Akizungumza na wananchi waliodhuria mkutano huo leo, Oktoba 18, Mama Samia amesema kuwa yupo kwa ajili yakumuwakilisha Rais Magufuli, ambaye amefanya kazi kubwa sana ya kuzunguka nchi nzima  na kuongea na wananchi.

 

“Niko hapa kwa niaba ya Mhe.Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambaye alitaka sana kuwa nanyi leo lakini kama mnavyojua tumefanya kazi kubwa yakuzunguka nchi tumeongea sana ameongea sana Dar es salaam, kwa kweli mpaka ananipigia simu nikamwambia Mheshimiwa pumzika mimi naenda" alisema Mama Samia

 

“Najua hivyo yuko ofisini anaendelea na kazi kwa hiyo nipo hapa kwa ajili yake na nitasema yale ambayo angekuwepo angesema na nitapokea yale ambayo mmeniambia niyabebe nimpelekee bila kuongeza wala kupunguza" aliongeza Mama Samia

 

Leo sekta binafsi imefanya makutano kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt.John Magufuli kwa mafinikio yaliyopatikana chini ya uongozi wake kwa muda wa miaka mitano huku Mama Samia Suluhu, akiwa mgeni rasmi akimuwakilisha Rais Magufuli.