Jumatatu , 17th Nov , 2014

Serikali imetakiwa kutoa elimu kwa Wavuvi wadogo wadogo wa Samaki kabla ya kuweza kuteketeza zana zao ikiwemo nyavu zao ili waweze kupata njia mbadala ya kuweza kufanya shguhuli zao za uvivu.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Abdulrahman Kinana.

Hayo yamezungumza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Abdulrahman Kinana wakati wa Ziara yake katika Mkoa wa Lindi Wilayani Kilwa na kuongeza kuwa
wananchi wanapaswa kuelemishwa kwanza na baada ya hapo ndipo wachukuliwe hatua endapo watakaidi amri.

Aidha Bw. Kinana ameitaka Serikali kushughulikia haraka Migogoro ya Ardhi ikiwemo kuwalipa fidia wananchi kwa wakati badala ya kuwazuia kufanya maendeleo kwa kisingizo cha kuchukua ardhi kwa kufanya maendelo ya Umma.

Aidha kinana amesema kama chama wanayohaki ya Kuikosoa serikali pale inapokikuka Ilani ya Chama ambayo ndio imewaweka madarakani na kusisitiza kuwa hakuna atakae weza kuikosoa serikali zaidi ya wao waliotoa ahadi kwa Wananchi.