Jumatano , 13th Nov , 2019

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, amesema Serikali iko kwenye majadiliano ya kununua ndege maalum kwa ajili ya kusafirishia mazao mbalimbali ikiwemo mbogamboga na matunda pamoja samaki kwenda nje ya nchi.

Waziri Kamwelwe ametoa kauli hiyo, leo Novemba 13, 2019, bungeni Dodoma, wakati akijibu swali kwa Mbunge wa Rombo, Joseph Selasin, ambaye alihoji juu ya kudhulumiwa kwa wananchi pindi wanapouza mazao, kutoka kwa wafanyabiashara wakigeni.

Mbunge Joseph Selasin ameuliza kuwa "jimboni Rombo tunalima Maparachichi na yananunuliwa na walanguzi kutoka Kenya, kwanini kama nchi tusinunue ndege ya mizigo ili kuwasaidia wakulima wetu kupeleka mazao nje ya nchi"

Akijibu swali hilo Waziri Kamwelwe amesema kuwa "tayari tumeshaanza kujadiliana ya namna ya kupata ndege ili kubeba mazao ya Horticultural (Matunda, Nyanya, kabeji, vitunguu, viazi), na tutaanza kwa kukodi ndege, baadaye tutanunua."