Alhamisi , 18th Jun , 2015

Serikali ya Tanzania imesema kuwa ipo katika mpango wa kukamilisha maabara katika shule za sekondari nchini na kuondokana na mtindo wa maabara za kuhamishika ili kutoa mafunzo ya halisi ya sayansi kwa shule zote za kata na za serikali.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa.

Akizungumza leo Bungeni katika kipindi cha maswali na majibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa amesema kuwa mahitaji ya nchi nzima kwa jumla maabara 10, 085 ambapo mpaka sasa maabara zilizokamilika ni 2,628 na 4,038 zipo katika hatua za ukamilishaji na zinazoendelea kujengwa ni 3,419.

Dkt. Kawambwa mkazo ambao wameuweka serikali kwa muongo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Jakaya Kikwete ni mpaka ifikapo mwishoni mwa mwezi wa Juni shule zote zitakuwa na maabara kamili na za kisasa na zenye vifaa vyote.

Katika hatua nyingine Mh. Kawambwa amesema serikali itaakaa na TCU, ili kuchukua wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi ambayo haya somo la Biology ili kujiunga na fani ya udaktari kama suala hilo halifanyiki sasa hivi.