Jumamosi , 9th Jan , 2016

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye amesema serikali ipo tayari kufanya mabadiliko ya muswada wa huduma ya habari ili kuridhia mapendekezo ya wadau wa habari.

Waandishi wa habari wakiwa katikia moja ya mikutano.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye amesema serikali ipo tayari kufanya mabadiliko ya muswada wa huduma ya habari ili kuridhia mapendekezo ya wadau wa habari.

Nnauye ameyasena hayo leo wakati alipokutana na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, ambapo ameahidi kuwa hakuna mapendekezo ya muswada huo ambayo yatapitishwa bila ya kukubaliana kwanza.

Aidha Nnauye amesema pia yupo tayari kusaidia mapendekezo ya wadau wa habari katika muswada wa haki ya kupata taarifa licha ya muswada huo kuwa chini ya wizara ya sheria ya katiba na sheria.