Jumamosi , 12th Sep , 2015

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Mussa, amesema serikali ina mpango wa kupunguza vizuizi vya barabarani ambavyo vinawekwa kiholela, na kuchangia kuzorotesha maendeleo ya ukuaji wa chumi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Mussa, akizungumza na wanahabari.

Akizungumza jana mkoani Mtwara katika semina ya kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji kwa maafisa biashara wa mikoa ya Lindi na Mtwara, amesema huo ni miongoni kwa mikakati iliyowekwa na wizara katika juhudi za kuondoa vikwazo kwa wafanya biashara.

Kwa upande wake, mkuu wa kitengo cha Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kutoka wizara hiyo, Sekela Mwaisela, amesema Tanzania imetajwa kuwa nyuma katika uanzishaji wa biashara ukilinganisha na nchi nyingine duniani na kujikuta nafasi ya 119 kati nchi 189 zilizofanyiwa utafiti na Benki ya dunia mwaka jana.

Naye, kaimu katibu tawala wa mkoa wa Mtwara, Johansen Bukwali, amewataka maafisa biashara hao kuyatumia vizuri mafunzo hayo, kwasababu hali ya uchumi wa mkoa huo inaelekea kukua kwa kasi na kwamba viwanda zaidi ya 40 vinatarajiwa kujengwa kutokana na kuwepo kwa rasilimali za gesi na mafuta.