
Wanawake katika kilimo, barani Afrika
Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam, katika Kongamano la Wanawake Wakulima Mery Mwakondo Gasper ambaye ni kaimu kamishna wa ardhi kutoka Wizara ya Ardhi amesema kutotumika kwa sheria hiyo kunaendelea kuwakandamiza wanawake na kubakia masikini.
Mwakondo amesema, mtazamo na mila potofu miongoni mwa jamii imetajwa kurudisha nyuma jitihada hizo hivyo ni jukumu la watendaji kutoa elimu kwa jamii kuachana na mila hizo sambamba na kuhimiza matumizi ya sheria hiyo.
Naye mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Bi Lilian Lihundi ameiambia East Africa Radio kuwa kongamano hilo linalenga kutoa tamko litakalo tumika barani Afrika na likilenga kumkomboa mwanamke Kijamii na kiuchumi.
Tamko hilo litakabidhiwa kwa viongozi wa Afrika mkoani Kilimanjaro tarehe 16 ya mwezi huu yaani Umoja wa Africa pamoja na Vyombo vya kikanda ikiwemo Umoja wa Maendeleo wa Nchi za Kusini mwa Afrika SADC na Jumuiya na Africa