Jumatano , 11th Feb , 2015

Waziri wa Nishati na Madini nchini Tanzania Mh. George Simbachawene amelitaka shirika la umeme nchini (TANESCO) kupunguza bei ya umeme kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.

Waziri wa Nishati na Madini Mh. George Simbachawene

Waziri wa Nishati na Madini nchini Tanzania Mh. George Simbachawene amelitaka shirika la umeme nchini (TANESCO) kupunguza bei ya umeme kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam leo mara baada ya kukutana na wafanyabiashara wa mafuta nchini Mh. Simbachawene pia ameishauri mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa
nchi kavu na majini SUMATRA kuona uwezekano wa kupunguza bei za nauli ili wananchi waone faida ya kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.

Amesema kwa kuwa bei hizo zinapopanda wananchi wamekuwa wakiilalamikia serikali, ni bora pia wakaishukuru serikali kwa kuonja manufaa ya kushuka kwa bei ya nishati hiyo.

Aidha katika hatua nyingine Waziri huyo wa nishati na madini ameitaka mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji nchini EWURA kuhakikisha inashirikiana na jeshi la polisi
kudhibiti uchakachuaji wa mafuta ambao kwa sasa umeonekana kufanyika na Ewura pekee bila ya kulishirikisha jesbi la polisi.