
Maagizo hayo yemetolewa leo na mratibu wa masuala ya jinsia kutoka Tamisemi Linus Kahandaguza pa moja na mkuu wa wilaya ya Ubungo Kheri James wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wataalam wa bajeti katika halmashauri kilichoandaliwa na mtandao wa jinsia nchini ambapo wamesema kwa sasa kumekuwa na ongezeko la vitendo vya ukatili nchini hivyo ni vyema kukachukuliwa hatua za haraka ikiwemo uundaji wa shwria hizo ndogondogo pa moja na uwekaji mipango katika bajeti za halmashauri zitakazo zingatia masuala ya usawa wa kijinsia .
Kwa upande wake mkurugenzi wa mtandao wa jinsia nchini lilian liundi pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya Same Yusto Mapande wamesema katika kikao hicho wamekutanisha madiwni na maafisa maendeleo na mipango kutoka halmashauri 14 ambapo watapata mafunzo juu ya namna ya kutenga bajeti zenye kulenga usawa wa kijinsia ambapo kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2016 zaidi ya dola za kimarekani bilioni 105 zimekuwa zikipotea kutokana na kutokuwepo bajeti za usawa wa kijisnia .
Nao baadhi ya madiwani kutoka halmashauri za Mbeya na Kishapu ambao wametajwa kuwa moja ya halmashauri zilizofanikiwa kutengeneza bajeti za usawa wa kijinsia wamesema halmashauri hizo zimefanikiwa kutenga fedha kwa ajili kutatua masuala ya usawa wa kijisnia ikiwemo kuja na shule maalumu za wasichana ..