Alhamisi , 27th Oct , 2016

Asilimia 25 ya watu duniani ambao wanaweza kufanya kazi ni vijana wakati katika ukanda wa Jangwa la Sahara asilimia 60 ya watu wanatakiwa kuwepo kazini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florens Turuka

Kwa Tanzania ni asilimia 6 pekee ya nguvu kazi ndiyo inayotumika ikiwa bado vijana wengi hawana ajira.

Takwimu hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florens Turuka wakati akizindua mpango wa taifa wa ushirikishaji vijana katika kilimo.

Amesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha kwa namna gani wanaweza kuwaondoa vijana nchi katika hali ya umaskini na kuwapatia ajira hivyo wamebuni sera na njia yakuwahusisha vijana katika shughuli za kilimo na tayari serikali inakamilisha maandalizi ya mpango wa maendeleo ya sekta ya kilimo mpango ambao utasaidia nchi isiingie kwenye baa la njaa.

Kwa upande wake muwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa la Charles Tulahi amesema kutokana na taifa kuwa na tishio uhaba wa chakula hivyo ni lazima nchi iweke nguvu kazi kubwa mwenye kilimo.