Jumatatu , 19th Feb , 2018

Katibu Mkuu Wizara wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Prof Elisante Ole Gabriel, amesema serikali itahakikisha viwanda vinavyobinafisishwa katika maeneo mbalimbali nchini vinafanya kazi kulingana na makusidi ya uanzishwaji wake.

Prof. Elisante ametoa kauli hiyo mkoani Kigoma mara baada ya kutembelea kiwanda cha Uvinza cha Nyanza, na kubaini kiwanda hicho kutofanya vizuri kutokana na kukosa mpango kazi uliothabiti.

Aidha katibu huyo amekitaka kiwanda hicho kutengeneza chumvi bora ambayo itaweza kuingia katika ushindani na baadhi ya watengenezaji wa chumvi hiyo huku wakiangalia gharama za uendeshaji wa kiwanda hicho cha chumvi.

Pia katibu huyo mkuu ameongeza kuwa wakati umefika kwa viwanda vilivyobinafisishwa nchini kufanya kazi kama inavyotakikana ili vianze kuchangia ukuaji wa uchumi moja kwa moja.