Jumatatu , 11th Nov , 2019

Waziri wa Katiba na Sheria, Augustine Mahiga, amewataka wananchi wasiokuwa na vyeti vya kuzaliwa kufika ofisi za Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), kwa ajili ya kujiandikisha na kupewa vyeti vyao vya kuzaliwa.

Waziri Mahiga ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma, leo Novemba 11, 2019, wakati wa kipindi cha maswali na majibu, ambapo amesema mpaka sasa Serikali kupitia RITA, wananchi mbalimbali wamepatiwa vyeti vya kuzaliwa ambavyo ni muhimu inapofika wakati wa mtu kuajiriwa.

Waziri Mahiga amesema "natoa wito kwa wananchi wote wasiokuwa na vyeti vya kuzaliwa kufika ofisi za Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), kwa ajili ya kusajiliwa na kupewa vyeti ya kuzaliwa."

Kwa sasa Bunge linaendelea jijini Dodoma, ambapo Mawaziri mbalimbali wanapata nafasi ya kujibu maswali kutoka kwa Wabunge.