
Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa wizara ya viwanda na biashara bwana Adelhel James Meru amsema serikali inapata hasara kubwa kwa kushindwa kuziongezea dhamani bidhaa jambo ambalo linapelekea kuzoretesha ukuaji wa teknolojia ya viwanda.
Bwana Meru ameeleza kuwa wizara yake kwa kushirikiana na wizara ya kilimo itahakikisha kuwa viwanda vya ndani vinajitosheleza kwa maligafi za kutosha ambapo kwa kuanza watajishugulisha na mazao ya pamba, alizeti, na uzalishaji wa ngozi.
Aidha amewataka wawekezaji wa viwanda kutambua kuwa serikali ina dhamira ya dhati ya kukuza uchumi wake kupitia viwanda na uzalishaji kwa kumtoa mtanzania kwenye kilimo duni hivyo upatikanaji wa maligafi ni mpango endelevu kwa mazao manne ya kwanza.