Jumatatu , 14th Nov , 2022

Mamlaka ya Uturuki imesema kwamba takriban watu sita wameuawa na wengine 81 kujeruhiwa katika mlipuko katika eneo lenye shughuli nyingi katikati mwa jinni la  Istanbul.

Mlipuko huo ulitokea mwendo wa saa za jioni Jumapili katika barabara ya manunuzi katika eneo la Taksim Square

Waziri wa mambo ya ndani wan chi hiyo amesema kwamba mshukiwa wa tukio hilo tayari amekamatwa,    mlipuko huo unadhaniwa kuwa shambulio la kigaidi lililotekelezwa na mwanamke mmoja.

Rais wan chi hiyo Recep Tayyip Erdogan amesema wahusika wataadhibiwa.Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Istanbul, alilaani kile alichokiita "shambulio baya" na kusema "harufu ya ugaidi" iko hewani.

Waziri wa sheria Bekir Bozdag ameviambia vyombo vya habari vya Uturuki kuwa mwanamke mmoja alikua amekaa kwenye benchi katika eneo hilo kwa zaidi ya dakika 40, na kuondoka dakika chache kabla ya mlipuko huo kutokea..