
Amesema lengo ni kuhakikisha kila Mtanzania anazifahamu, kuzitii na kuzitekeleza sheria hizo
Waziri Ndumbaro ameyasema hayo, Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliochangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo ikiwemo hoja ya utoaji wa elimu kwa Wananchi juu ya matumizi ya haki zao kwenye katiba na sheria za nchi, hoja iliyotolewa na mbunge wa Mwanga, Mhe. Joseph Tadayo.
"Serikali kupitia wizara ya katiba na sheria imejipanga kila Mtanzania aweze kuelewa sheria, kutekeleza sheria na kuzitii sheria, ili suala la kutojua sheria lisiwe la utetezi na liweze kuondoka kabisa," alifafanua Dkt. Ndumbaro.
Aliendelea kusema kuwa, katika kuhakikisha kila Mtanzania anazifahamu, kuzitii na kuzitekeleza sheria, wizara imejikita kutafsiri sheria kwenye lugha ya kiswahili