
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sihaba Nkinga.
Akizungumza katika kongamano la watoto la kuadhimisha siku ya kimataifa ya mtoto wa kike lililofanyika katika shule ya Mwendakulima wilayani Kahama, Nkinga amesema vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vimekithiri ambavyo hivi sasa mkoa wa Shinyanga unaongoza kwa matukio hayo.
Nkinga amesema kwa mkoa huo wa Shinyanga unaongoza kwa asilimia 59 ya watoto wa kike kuolewa na kupewa mimba wakiwa chini ya umri wa miaka 18 hali inayowafanya kukosa haki zao za msingi ikiwemo elimu.
Kilele cha siku ya mtoto wa kike kitaifa kitafanyika leo Mkoani Shinyanga ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na watoto,ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mimba na ndoa za utotoni zinaepukika chukua hatua kumlinda mtoto wa kike.