Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Siasa ni shule isiyokuwa na mwisho - Kikwete

Jumapili , 26th Feb , 2017

Mbunge wa Chalinze mkoani Pwani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwan Kikwete, amesema siasa ni shule ambayo haina mwisho na ndiyo maana anaendelea kujifunza mengi kutoka kwa wanasiasa wenzake husani waliomtangulia bila kujali chama.

Ridhiwan Kikwete akiongea na Edward Lowassa katika uwanja wa Taifa

Kikwete ametoa ujumbe huo mara baada ya kukutana na kuteta na alikuwa mgombea urais kupitia CHADEMA katika uchaguzi wa mwaka 2015, Edward Lowassa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga.

Kikwete ambaye ni mwanachama na kiongozi ndani ya klabu ya Yanga, alimfuata Lowassa alipokuwa amekaa na kufanya naye mazungumzo ambayo hajayaweka wazi, na kisha kurudi sehemu yake huku akishuhudia timu yake ya Yanga ikilala mabao 2-1.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kikwete ameandika "Siasa ni shule ambayo haina mwisho. nahisi bado niko shule ya msingi na ninaendelea kujifunza".

Ridhiwan Kikwete akimvuta mkono Freeman Mbowe, walipokutana kwenye uwanja wa Taifa 

Pia mbunge huyo alitumia fursa ya mchezo huo kukutana na mbunge wa Hai ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na kuzungumza naye mawili matatu.

Kikwete na MBowe wote ni wapenzi wa Yanga, kwahiyo bila shaka wote waliondoka uwanjani hapo wakiwa na majonzi ya kipigo kutoka kwa Simba.

Mbali na hao, mechi hiyo pia iliwakutanisha mahasimu wengine katika siasa za Bongo, ambao ni Nape Nnauye na Edward Lowassa waliokuwa wamekaa katika eneo moja, ambapo Nap ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika mchezo huo

HABARI ZAIDI

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu

Mwili wa Boaz Sanga, Mwanafunzi wa CHuo cha SAUTI Mwanza baada ya kupatikana Pembezoni wa Ziwa Viktoria

Mwanafunzi wa SAUTI afariki akijaribu kuogelea

Luteni Jenerali Charles Muriu Kahariri, CDF Mpya wa Kenya

Luteni Charles Muriu ateuliwa kuwa CDF mpya Kenya

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa 124%

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita