
Nape ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Mwanza, kwenye kilele cha Tamasha la Urithi Festival, ambapo amesema hajapunguza kasi kama ambavyo watu wanadai bali kwa sasa ndiyo ananguvu kubwa zaidi ya kuzungumza na kufanya maamuzi.
"Kwanza kasi haijapungua ni hisia za watu, sasa hivi ninauzoefu zaidi, kasi zaidi na nguvu zaidi mengine kama wanataka tusubiri wakati Bunge linaanza Jumanne, tutegemee kasi zaidi katika kuwatumikia wananchi wa Mtama" amesema Nape
"Kwa sasa naweza kuongea na Ris moja kwa moja, kusimama Bungeni kiufupi Nape anayeweza kusimama Bungeni ni yuleyule mwenye msimamo" amesema Nape
Hivi karibuni Rais Magufuli akiwa mkoani Lindi alimsifia kiongozi huyo na kusema anampenda sana, kwa kuwa ni kiongozi bora na wakuigwa kwenye Mkoa huo.