Waliowasili hivi karibuni wote walikuwa katika wiki za mwisho za ujauzito, kulingana na shirika la kitaifa la uhamiaji.
Inaaminika kuwa wanawake hao wanataka kuhakikisha watoto wao wanazaliwa nchini Argentina ili kupata uraia wa Argentina.
Idadi ya wanaowasili imeongezeka hivi karibuni, ambayo vyombo vya habari vya ndani vinapendekeza ni matokeo ya vita nchini Ukraine..
Kati ya wanawake 33 waliowasili katika mji mkuu wa Argentina kwa ndege moja siku ya Alhamisi, watatu walikamatwa kwa sababu ya "matatizo ya nyaraka zao", wakiungana na wengine watatu waliowasili siku iliyopita, mkuu wa shirika la uhamiaji Florencia Carignano aliambia La Nacion.
Wanawake wa Urusi awali walidai kuwa walikuwa wakitembelea Argentina kama watalii, alisema
"Katika matukio haya ilibainika kuwa hawakuja hapa kujihusisha na shughuli za utalii. Walikiri wenyewe."
Alisema wanawake wa Urusi walitaka watoto wao wawe na uraia wa Argentina kwa sababu ilitoa uhuru zaidi kuliko pasipoti ya Urusi

