Jumamosi , 10th Jun , 2017

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini , IGP Simon Sirro amewataka Watanzania wawe wavumilivu kwa kuwa Polisi wanafanya uchunguzi wa kina kuhusu mauaji yanayoendelea mkoani Pwani.

IGP Sirro amesema hayo leo katika ziara yake ya kwanza mkoani Morogoro tangu ateuliwe na kuapishwa kuwa IGP ili kuzungumza na polisi namna ya  kusimamia ulinzi na usalama.

Amesema kuwa, "Hatulali  jeshi linafanya kazi kwa juhudi kubwa nawaomba sana wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi ili kuweza kuwabaini wahalifu hao ambao wanatekeleza vitendo vya mauaji katika mkoa wa Pwani. Ikiwa ni pamoja na kusaidia kudumisha hali ya usalama nchini na nyie waandishi wa habari mnatakiwa  kuandika taarifa kwa kuzingatia weledi na maadili ya taaluma pasipo kuleta uchochezi." IGP Sirro alisisitiza

Aidha Kamanda Sirro amesema kuwa amefanya ziara hiyo Morogoro na sehemu zingine nchini ili kuzungumza na jeshi la polisi namna ya kusimami ulinzi na usalama katika maeneo yao.