Jumanne , 29th Oct , 2019

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameyakamata magari mawili moja basi la abiria, na lori yaliyotaka kusababisha ajali kwa kufukuzana na kuovateki bila ya kuwa na tahadhari katika barabara kuu ya Mwanza Mara.

Waziri Kangi Lugola (kushoto) akimhoji dereva wa moja ya basi alilolikamata.

Tukio hilo limetokea Wilayani Busega Mkoani Simiyu, leo Oktoba 29, 2019, wakati Waziri Lugola alipokuwa safarini akitokea Mjini Bunda, Mkoani Mara, na magari hayo yakitokea Mwanza yakiwa na mwendokasi ndipo yakaanza kuovateki bila kuwa na tahadhari na kusababisha magari mengine yaliyokuwa yanakuja mbele ya magari hayo likiwemo la Waziri huyo kuanza kupoteza uelekeo kwa kuyakwepa magari hayo.

Baada ya tukio hilo, Waziri huyo alimwelekeza dereva wake kugeuza gari na kuyakimbiza magari hayo hasa basi hilo Manoni Safaris lenye namba za usajili T800DCU, ambalo ndilo lililokuwa na makosa kwa kulazimisha kuovateki wakati gari alilokuwa analifukuza aina ya Kenta lenye namba za usajili T865CVJ likiwa limeovateki kwa usalama.

Waziri huyo alimkamata dereva wa basi hilo na kumtaka atoe leseni yake, kabla ya kupelekwa Kituo cha Polisi Busega kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka, na alielekeza abiria wa basi hilo warudishiwe nauli zao na watafutiwe basi lingine ili waendelee na safari.

Zaidi tazama Video hapo chini