Jumatano , 22nd Apr , 2015

Ofisi ya Rais Ufutiliaji wa Utekelezaji wa miradi PDB, inayosimamia Mpango wa Matokeo Makubwa sasa BRN, imealika wataalamu wa kilimo kuchambua na kutoa mapendekezo juu ya namna bora nchi inavyoweza kutatua changamoto ya masoko kwa wakulima.

Mtendaji mkuu wa PDB, Omary Issa.

Akifungua maabara ndogo ya siku tano ili kutathimini mifumo ya sasa ya masoko mtendaji mkuu wa PDB, Omary Issa amewataka wadau wote husika kufanya kazi kwa pamoja katika kuleta majibu yanayolenga mikakati ya muda mfupi na mrefu kwa wakulima.

Bw. Issa amesema nidhamu ya kiutendaji ya BRN, inawataka wadau wa sekta za umma, na binafsi kufanya kazi kwa pamoja ili kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo muhimu na kusema majibu ya utatuzi wa masoko yatatoka kwenye pande hizo mbili.

Maabara hiyo ndogo inahusisha wawakilishi 50 kutoka sekta za umma, binafsi, taasisi za kimataifa na wakulima wenyewe.

Tanzania nzima husususani miradi ya kipaumbele ya kilimo iliyo chini ya BRN, ilihsuhudia uzalishaji mkubwa wa mahindi na mpunga kwa msimu wa mwaka 2013/2014 jambo ambalo limeleta fursa nzuri lakini likapambana na changamoto ya masoko.