Spika Mstaafu awapongeza CHADEMA kwa hili

Jumatatu , 18th Mei , 2020

Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa, amesema kuwa CHADEMA wako sahihi kuwafukuza wanachama wake ambao wameenda kinyume na taratibu zao kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania, Pius Msekwa.

Mzee Msekwa ameyabainisha hayo alipofanya mazungumza maalum na EATV&EA Radio Digital.

"Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kiko sahihi kuwafukuza wabunge wake kutoka kwenye chama hicho, hivyo mamlaka hayo wanayo kwa mujibu wa katiba ya chama" amesema Mzee Msekwa.

Hivi karibuni CHADEMA kupitia kwa Katibu wa chama hicho John Mnyika, kiliwafukuza uanachama wabunge wake wanne, akiwemo David Silinde, Anthony Komu, Wilfred Lwakatare na Joseph Selasini, baada ya kukiuka maagizo na maelekezo ya chama.