Jumanne , 8th Sep , 2015

Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), chini ya Mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Mh. Edward Lowassa , amesema amekwishakamilisha mipango ya kuondoa kero zinazowakabili wakazi wa Dar es Salaam.

Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),chini ya Mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),Mh. Edward Lowassa akihutubia mkutano Kibamba

Akizungumza katika viwanja vya Bunju katika Jimbo la Kawe Mkoani Dar es Salaam Mh. Lowassa amesema siku zilizobaki kwa ajili ya kupiga kura watanzania watafakari kama wanataka kuendelea na matatizo waliyonayo kwa miaka 50 au wachague ukawa ili wawataliwe matatizo yao.

Mh. Lowassa amesema anajua matatizo yanayowakabili wakazi wa Dar es Salaam ikiwemo kero ya usafiri kutokana na foleni, ukosefu wa maji, tatizo la ajira kwa vijana na mengineyo.

Aidha Mh. Lowassa amewataka wananchi wakapige kura kwa kuwahakikishia hakuna kura itakayoibiwa hivyo wasikose usingizi kwa kufikiri kura zao ambazo watapiga ili kumpa ridhaa ya kuingia Ikulu.

Aidha Lowassa amesema kuwa watu wapo maofisini ambao wanataka kujiunga na vuguvugu la mabadiliko lakini wanatishwa huku wafanyabiashara wakitishiwa pindi watakapousaidia umoja huo katika harakati zake.