Ijumaa , 24th Mar , 2023

Chama cha wanasheria Tanganyika TLS kimetangaza Mkutano Mkuu wake ambao utakuwa na Uchaguzi wa nafasi mbalimbali ikiwemo ya Rais ambapo Harold G Sungusia na Reginald Shirima wamepitishwa kuwania nafasi hiyo, inayoshikiliwa na Dkt. Edward Hosea anayemaliza muda wake

Wagombea wote waliopitishwa na kamati wanaweza kuanza kampeni kuanzia Machi 27 na Mkutano Mkuu utafanyika Mei 11-13, 2023 jijini Arusha 

Taarifa ya TLS imesisitiza kuwa Wakati wote wa kampeni wagombea wote kufanya kampeni za kistarabu kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria za uchaguzi za chama.

Hata hivyo imeeleza kuwa wale wote ambao hawajarizishwa na maamuzi ya kamati ya uchaguzi,  wanatakiwa kukata rufaa kwenye  Electoral Appeals Committee kwa mujibu wa  sheria, kanuni na taratibu zilizopo