Jumatano , 3rd Dec , 2014

Taasisi muhimu za miundombinu za Wizara ya Mawasiliano ya Zanzibar ambazo zinagusa jamii ziko katika hali isiyoridhisha na kusababisha wananchi wengi kukosa huduma kutoka taasisi hizo za serikali.

Waziri wa Miundombinu na Mawasialino wa Zanzibar Mh. Juma Duni Haji

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Miundombinu na Mawasialino wa Zanzibar Mh. Juma Duni Haji wakati akizungumza na watendaji wa mamlaka za usafiri baharini, mamlaka ya viwanja wa ndege na bodi ya bandari na ile ya shirika la meli la Zanzibar mkutano ambao umefanyika visiwani humo ukiwa pia ni wa kuzinzindua bodi mpya za taasisi hizo.

Mh. Duni amesema ameshuhudia taasisi nyingi zina ukosefu wa vitendea kazi, utaalamu na bajeti finyu hali inayosababisha utendaji na uwajibikaji kuwa katika hali ngumu.

Mapema Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Haji Gavu amesema kuna haja ya taasisi hizo kukutana na kukaa pamoja kwa vile hiyo ndiyo moja ya njia ya watendaji kujuana na kuwa na mikakakati ya pamoja na itakayosaidia kuondosha mivutano ya taasisi hizo zilizo ndani ya wizara mmoja.

Taasisi hizo za serikali zilizokutana na waziri ni pamoja na idara za barabara, leseni na bodi za bandari, mamlaka ya usafiri baharini na viwanja wa ndege.