''TANESCO mkinizingua tutazinguana'' - RC Mndeme

Jumatano , 21st Apr , 2021

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi. Christina Mndeme ameitaka TANESCO mkoa huo kutokuwa chanzo cha kikwazo cha wananchi kupata maji safi na salama baada ya mradi wa muda mrefu ambao upo katika halmashauli ya Madaba kukamilika.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi. Christina Mndeme

Amesema mradi huo umekamilika lakini kikwazo kipo katika shirika hilo kupeleka umeme ili wananchi wa Halmashauli hiyo waondokane na kero kubwa ya maji ambayo wanaipata.

''Nataka Alhamisi wiki ijayo maji yaanze kutoka, TANESCO mkinizingua tutazinguana, na atakayenikwamisha awe TANESCO au RUWASA ama mtu yeyote mwenye nia mbaya Tutazinguana,'' amesema Bi. Mndeme.

Mradi huo wa maji upo katika Halmashauri ya Madaba iliyopo wilaya ya Songea mkoani Ruvuma na serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 2.

Zaidi tazama video hapo chini